SERIKALI YATOA TSH BIL 99.3 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO GEITA
GEITA
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya bilioni 99.3 kwa mkoa wa Geita kwa lengo la kuendelea kutekeleza miundombinu mbalimbali ya kimaendeleo kwa lengo la kusogeza huduma za msingi kwa Wananchi katika sekta ya Afya , Elimu, maji na miundombinu ya Barabara.