DKT SAMIA APANDISHA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA KWA 35.1%
SINGIDA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameongeza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa serikali kwa asilimia 35.1.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo Mei 1, 2025 wakati akihutubia kwenye maadhimisho yasiku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Singida.
Rais Samia amesema" Baada ya kuangalia uchumi ulivyopanda na umepanda kwa sababu ya nguvu zenu wafanyakazi , ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba katika kuzidi kuleta usawa kwa wafanyakazi mwaka huu serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwaasilimia 35.1"
Dkt Samia ameongeza "nyongeza hii itakayoanza kutumika mwezi julai mwaka huu itaongeza kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi laki tatuna sabini hadi shilingi laki tano(370,000-500,000)"
Aidha Mhe.Rais ameongeza kuwa ngazi zingine za mishahara zitapanda kwa kiwango kizuri kutokana bajeti itakavyoruhusu.