TSH MIL 339 ZAJENGA MADARASA NA VYOO CHAFUKWE
NJOMBE
Serikali imeipatia shule ya sekondari Mt.Chafukwe iliyopo katika Kata ya Mfumbi Halmashauri ya wilaya Makete Mkoa wa Njombe kiasi cha shilingi milioni 339 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba12 vya madarasa na matundu ya vyoo 20 ili kuendelea kuimaisha miundombinu ya elimu katika Mkoa huo.