MRADI WA TSH BIL 185 KUWATUA NDOO MOROGORO
MOROGORO
Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) imeanza kutekeleza mradi wa maji wenye thamani ya Sh bilioni 185 kwenye Manispaa ya Morogoro Mkoa wa Morogoro.
Fedha hizo zinatokana na serikaki chini ya ufadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), kuboresha Bwawa la Mindu na miundombinu ukiwemo ujenzi wa mtambo wa kutibu maji eneo la Mafiga.
Aidha Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2021/22 hadi 2025/26 umeweka kipaumbele katika upatikanaji na usambazaji wa majisafi na salama vijijini na mijini na utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira.
KUMBUKA:- Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (2020-2025) imeielekeza serikali kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa mijini inakuwa 95% na vijijini inakuwa 85% ifikapo mwaka 2025.