TSH BIL 8 KUJENGA BWAWA LA UMWAGILIAJI BARIADI

samia simiyu

TSH BIL 8 KUJENGA BWAWA LA UMWAGILIAJI BARIADI

 SIMIYU

Serikali ya awamu ya sita  katika kukuza kilimo cha umwagiliaji nchini imeidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la umwagiliaji la Kasoli lililopo katika Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.

Ujenzi wa bwawa hilo umefikia 40% na unatakiwa kukamilisha ifikapo Julai 2024., na utakapokamilika Utawanufaisha wakulima zaidi ya 720 na kuwasaidia kuongeza tija ya uzalishaji wa mahindi na mpunga.