KUANZISHA MFUMO WA M-MAMA

 

KUANZISHA MFUMO WA M-MAMA

KUANZISHA MFUMO WA M-MAMA

Mfumo wa M-Mama, unaoratibu usafiri wa dharura kwa akina mama na watoto wachanga, umefanikiwa kuokoa maisha ya watu zaidi ya 5,000 tangu ulipoanzishwa, kwani zaidi ya akinamama na watoto wachanga 120,000 wamesafirishwa kwa dharura kupitia mfumo huo. 
Aidha,Mfumo wa M-Mama umeondoa changamoto ya ukusanyaji wa data, ambapo awali taarifa za rufaa zilihifadhiwa ndani ya vitabu vya usajili kwenye vituo vya afya. Sasa taarifa hizi zinapatikana kwa urahisi kupitia mifumo yetu ya kidigitali.
Jumla ya watoa huduma 20,000 wanapewa mafunzo rasmi na elekezi kazini kupitia mpango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili kuhakikisha huduma za afya kwa mama na mtoto zinaimarishwa.
Kupitia mpango huu, Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha huduma za afya kwa watoto wachanga na akina mama zinaboreshwa zaidi, huku lengo likiwa ni kupunguza vifo zaidi na kuimarisha ustawi wa familia nchini
#BimkubwanaAfyakazini