DKT SAMIA AENDELEA NA ZIARA VISIWANI ZANZIBAR
ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara ya kichama iliyoanza Januari 17 2024 yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya kichama ya maendeleo na kuzungumza na Viongozi, Wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Katika muendelezo wa ziara hiyo Mhe Dkt Samia leo Januari 18 ametembelea jimbo la Paje na pichani ni wakati akisalimiana na wananchi wa jimbo la Paje waliojitokeza barabarani wakati wa ziara hiyo.
Aidha Ziara hiyo inafanyika katika Mikoa minne ambayo ni Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini na Mkoa wa Magharibi.
