TSH BIL 116 KUONGEZA NGUVU NFRA NA CPB

SAMIA,DAR ES SALAAM

TSH BIL 116 KUONGEZA NGUVU NFRA NA CPB

 DAR ES SALAAM.

Serikali ya awamu ya sita imetoa shilingi bilioni 116 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) ili kuchochea soko, ambapo katika awamu ya kwanza, NFRA imenunua jumla ya tani 200,293 za mazao.

Aidha Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 17,148,290 msimu wa 2021/2022 hadi tani 20,402,014 msimu wa mwaka 2022/2023, hivyo kufikisha 124% ya kiwango cha utoshelevu wa chakula nchini.