RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO MAALUM YA KIMATAIFA YA THE GLOBAL GOALKEEPER AWARD
Kwa kutambua namna ambavyo Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameonesha juhudi kubwa kwenye sekta ya afya nchini tangu alipoingia madarakani Machi 2021, Taasisi ya Gates mnamo Februari 4, 2025 Ilimtunuku tuzo Maalum ya Kimataifa ya THE GLOBAL GOALKEEPER AWARD,tuzo ambayo aliipokea jijini Dar es salaam kupitia kwa Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates, Dkt. Anita Zaidi ikiwa ni kama kielelezo cha matokeo makubwa ambayo yamepatikana kwenye uongozi wake kufuatia ripoti ya utafiti wa demografia na afya ya mwaka 2022 inayoonesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80 hapa Nchini.
Mhe. Rais Samia ndiye kiongozi wa kwanza kupokea tuzo hiyo kwa bara la Afrika jambo lililochochewa na uongozi wake mahiri ulioleta mafanikio makubwa nchini hususani ni sekta ya afya kwa kuitendea haki na kusababisha mataifa makubwa duniani kutambua mchango wake.
Mafanikio haya yametokana na mikakati mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kutokana na utashi wa kisiasa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia kuweka mazingira wezeshi kisera pamoja na kuimarisha rufaa za akina mama na watoto pamoja na kuongeza bajeti ya kuimarisha huduma ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kusogeza huduma za dharula za uzazi karibu na wananchi kwa kujenga zaidi ya vituo 530 vya upasuaji wa kutoa mtoto tumboni.
#BimkubwanaAfyaKazini