TSH BIL 3 ZAJENGA HOSPITALI YA WILAYA MISUNGWI
MWANZA
Serikali ya awamu ya sita imeidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya Misungwi iliyojengwa katika kijiji cha Iteja Mkoani Mwanza.
Kiasi hicho cha fedha kimefanikisha ujenzi wa majengo zaidi ya 14, kukamilika kwa hospitali hiyo kumewarahishia wananchi wa maeneo hayo ambao hapo awali walilazimika kuifata kwenye kituo cha Afya Mitindo kilicho umbali wa Kilomita 8.