TANZANIA YAPONGEZWA KUDHIBITI UHARAMIA BAHARI YA HINDI

 

tanzania yapongezwa kudhibiti uharamia bahari ya hindi

TANZANIA YAPONGEZWA KUDHIBITI UHARAMIA BAHARI YA HINDI

DAR ES SALAAM
Tanzania,Msumbiji na Djibouti zimepongezwa kwa ushirikiano wao katika kukabiliana na changamoto za usalama wa baharini zilizosababisha kupungua kwa uharamia katika ukanda wa Bahari ya Hindi.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Kamanda wa Ushirikiano wa Kijeshi  Africom ya Marekani, Balozi Robert Scott jijini Dar es Salaam januari 24 kwenye semina ya siku nne inayohusisha washiriki wa kijeshi na raia iliyoanza Jumatatu wiki hii iliyoandaliwa na Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati cha Afrika.
Amb Scott amesema"Tunathamini ushirikiano wa Tanzania katika uwanja wa usalama wa baharini, tumetoka mbali, na pamoja na washirika wengine barani Afrika kama Msumbiji na Djibouti kwa pamoja tumepunguza uharamia. Hali ilikuwa mbaya zaidi siku za nyuma kuhusu shughuli haramu,” 
Africom inafanya kazi katika maeneo matatu ambayo ni Diplomasia, Maendeleo na Ulinzi na lengo lake ni kuwezesha uchumi wa bluu na kupanua wigo wa kuamua  kuzuia usafirishaji haramu baharini, biashara haramu ya binadamu na biashara haramu ya wanyamapori.