TANZANIA NA ANGOLA ZASAINI MoUS TATU

 

TANZANIA NA ANGOLA ZASAINI MoUS TATU

TANZANIA NA ANGOLA ZASAINI MoUS TATU

ZANZIBAR

Tanzania na Angola zimesaini Hati tatu za Makubaliano ya Ushirikiano (MoUs) katika sekta ya mafuta na gesi, kuondoleana visa kwa wenye hati/pasi za kusafiria za kidiplomasia na za kikazi pamoja na ushirikiano katika sekta ya afya.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wizara ya afya na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Balozi Téte António wakati wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Angola uliofanyik siku za hivi karibuni Zanzibar.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesaini hati mbili za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya mafuta na gesi na kuondoleana visa/pasi kwa wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na za kikazi.

Aidha Tanzania na Angola zina uhusiano wa kihistoria ulioanzishwa na viongozi wakuu wa Kitaifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Agostinho Neto walianzisha uhusiano huo kwa matarajio yao kuwa uhusiano huo utoe manufaa kwa nchi zote mbili.