RIPOTI YA IMF:TANZANIA HAINA MADENI ZAIDI BARANI AFRIKA
WASHINGTON, D.C
Kwa mujibu wa ripoti kutoka shirika la fedha Duniani (IMF) kuhusu mtazamo wa Kiuchumi wa Kikanda inasema TANZANIA ndiyo nchi inayoongoza kwa kutokuwa na deni kubwa barani Afrika kutokana na kuwa kinara wa uwajibikaji wa kifedha, ikijivunia uwiano wa deni kwa Pato la Taifa wa 41.8%.
Mafanikio hayo yanaonesha mtazamo wa kifedha wenye busara na uwiano ambao unachangia kwa kiasi kikubwa utulivu na uthabiti wa uchumi wa nchi.Uwiano wa deni kwa Pato la Taifa ni kipimo muhimu ambacho kinalinganisha jumla ya deni la nchi na pato lake la kiuchumi.
Kutokana na ripoti hii ya IMF inaonesha kwamba Tanzania ina uwezo wa kupata mikopo kutoka kwa wafadhili wa maendeleo na kuwahudumia.