HATUA ZILIZOPIGWA KWA MIAKA MINNE YA MHE. RAIS SAMIA KWENYE MIUNDOMBINU KUPITIA TANROADS

 

HATUA ZILIZOPIGWA KWA MIAKA MINNE YA MHE. RAIS SAMIA KWENYE MIUNDOMBINU KUPITIA TANROADS

HATUA ZILIZOPIGWA KWA MIAKA MINNE YA MHE. RAIS SAMIA KWENYE MIUNDOMBINU KUPITIA TANROADS 

Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, jumla ya kilomita 15,625 za barabara zimekuwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji, ambapo wameweza kujenga na kukamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye jumla ya kilomita 1,365 na kilomita nyingine 2,031 zipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi wa kiwango cha lami.
Kilomita 2052.9 za barabara na madaraja mawili yamekwishafanyiwa upembuzi yakinifu na tayari yapo kwenye hatua za ujenzi kwa kiwango cha lami, na kilomita 4,734 na madaraja kumi upembuzi unaendelea
Madaraja mengine saba pamoja na kilomita 5,326 za barabara zipo katika maandalizi ya kufanyiwa upembuzi ili zijengwe kwa kiwango cha lami.
Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imekamilisha ujenzi wa barabara 25 zenye jumla ya kilomita 1,198 ambapo jumla ya shilingi trilioni 1.68 zimetumika kwa barabara hizo kukamilika kwa 100%.
Pia serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi 52  ya ujenzi wa barabara na madaraja kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS)  ambapo kwa kuongeza barabara 25 zilizokamilka inafanya kuwa  na miradi 77 ya barabara na madaraja huku thamani ya miradi yote kufikia Shilingi Trilioni 4.6
Aidha, hali ya barabara katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarika, ambapo barabara zilizopo katika hali nzuri ya wastani imeongezeka kutoka 88% hadi 90% hivi sasa
MUHIMU:- kutokana na mafanikio ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja nchini imeifanya Tanzania kuwa nafasi ya 6 kati ya nchi 54 za Afrika kuwa na mtandao bora wa barabara ikipanda kutoka nafasi ya 16 iliyokuwapo katika mwaka 2022 kulingana na Takwimu za Statista.com

#bimkubwanamamboyandanikazini