TSH MIL 174. 3 ZAWAPA MAJI WAKAZI 6,000 WA KILOSA
MOROGORO
Kiasi cha shilingi milioni 174.3 kimetumika kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji katika kijiji cha Ulaya Kibaoni Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na kuwaongezea upatikanaji wa maji kwa wakazi 6,000 wa maeneo hayo.
Ujenzi wa mradi huo ulianza Aprili 2024 na kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa tanki kuu la maji lenye ujazo wa lita 50,0000 juu ya mnara wa mita sita ikiwa na miundombinu ya kutibu maji na ujenzi wa vituo vitano wa kuchota maji,uzio wa nyumba ya mtambo na ufungaji wa mfumo wa umeme juu kwenye chanzo cha maji.
Ukamilikaji wa Mradi huo unalenga kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo hususan wanawake na watoto ambao walikuwa wakikumbwa na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.