DKT SAMIA AZINDUA CHUO CHA USHONAJI CHA WANAWAKE MAHONDA

 ZANZIBAR 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan amezindua Chuo cha wajasiriamali Wanawake Mkoa wa Kaskazini Unguja Cha Jumuiya ya Wanawake UWT ambacho ujenzi wake umegharimu Shilingi Milioni 72 na kitatoa mafunzo kwa Wanawake.

Akizindua chuo hicho Rais Dkt, Samia ameahidi kutoa Cherehani za kisasa Tano kwa ajili ya Kusaidia Shughuli za kijasiriamali chuoni hapo hatua ambayo litasaidia kuongeza ajira kwa Wanawake hao.