ELERAI NA LULAGO ZAPATIWA TSH MIL 100 UJENZI WA ZAHANATI

ELERAI NA LULAGO ZAPATIWA TSH MIL 100 UJENZI WA ZAHANATI 

TANGA

Serikali katika kuhakikisha huduma za kijamii ikiwemo afya zinasogezwa karibu na wananchi imeipatia Halmashauri ya wilaya Kilindi mkoani Tanga kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati katika vijiji vya Elerai na Lulago.

Majengo hayo ya zahanati ya kijiji cha Elerai kilichopo kata ya Kibirashi na Lulago kilichopo kata ya Lwande yalianza kujengwa kwa kutumia nguvu za wananchi na serikali imetoa kiasi hicho cha fedha ili kuunga mkono jitihada za wananchi wake Fedha hizo zitasaidia wananchi hao na Halmashauri nzima kuendelea kuboresha miundombinu ya afya na kuisaidia jamii hususani wakina mama wajawazito na watoto wanaotaabika kutembea umbali wa kilomita 8 kufuata huduma za afya.