DKT SAMIA AGAWA BOTI ZA KISASA KANDA YA ZIWA MWANZA

 

DKT SAMIA AGAWA BOTI ZA KISASA KANDA YA ZIWA  MWANZA

DKT SAMIA AGAWA BOTI ZA KISASA KANDA YA ZIWA 

MWANZA

Mhe Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan amegawa Boti za Kisasa kwa Wavuvi wa Kanda ya Ziwa, boti ambazo zimetolewa kwa mkopo usio na riba ili kuwawezesha kufanya Biashara ya Samaki kwa tija, Zoezi ambalo limefanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024

Akizungumza na wananchi wa Mwanza katika uwanja wa Nyamagana Dkt Samia ameitaka wizara ya mifugo na uvuvi kushirikiana ja sektetarieti za mikoa na Halmashauri kudhibiti na kutokomeza vitendo vya uvuvi haramu.

Aidha Mhe Rais Samia amesema kundi la vijana na wanawake linaongoza kushiriki kwenye ajira zisizo rasmi hivyo serikali inarasimisha shughuli zao kwa kuwawezesha kupata zana na nyenzo za kisasa ili kujikimu kiuchumi.

ZINGATIA: Jumla ya boti 55 zimegawiwa kwa wavuvi 989 kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa. (Mwanza boti 26) (Mara boti 11)  (Geita boti 9)  na Kagera boti 8.

#MAIKHALIIKANDAYAZIWA