MEGAWATI 4,031.44 ZAUNGANISHWA GRIDI YA TAIFA
TANZANIA
Hadi Machi 2025 Serikali ya awamu ya sita imefanikisha kuunganisha megawati 4,031.44 za umeme kwenye gridi ya taifa ikilinganishwa na Megawati 1,889.84 za Februari, 2024.
Ongezeko hilo limetokana na kukamilika kwa baadhi ya miradi ya kuzalisha umeme ikiwemo Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (megawati 2,115) na Rusumo – Nyakanazi (megawati 26.6),
Ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa umeme unaowafikia wananchi, Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme ambapo hadi Februari, 2025, njia ya kusafirishia umeme imeongezeka na kufikia urefu wa kilomita 8,025.38 kutoka kilomita 7,745.38 zilizokuwepo mwaka 2024.
Vilevile, njia za kusambaza umeme zimeongezeka na kufikia urefu wa kilomita 198,215.17 ikilinganishwa na kilomita 176,334.14 zilizokuwepo.