MSUMBIJI KUJIFUNZA UTAALAMU WA MATIBABU JKCI

 

MSUMBIJI  KUJIFUNZA UTAALAMU  WA MATIBABU  JKCI

MSUMBIJI  KUJIFUNZA UTAALAMU  WA MATIBABU  JKCI 

TANZANIA
Jamhuri ya Msumbiji itashirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete( JKCI) kwa kuwatuma wataalamu wake kujifunza namna ya kutoa huduma za matibabu ya moyo  kwa wagonjwa ili nchi hiyo iwe uwezo wa kutoa huduma hizo kwa wananchi wake.
Ushirikiano mwingine ni wa kuwapeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa katika Taasisi hiyo na kuwatuma wataalam wao kwenda kujifunza namna ya kutoa huduma za matibabu ya moyo na hiyo ni sehemu ya tiba utalii.
Hayo yamesemwa   Mei 8, 2025 na Mke wa Rais wanchi hiyo Mhe. Mama Gueta Selemane Chapo alipotembelea taasisi hiyo  iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa ikiwa ni sehemu ya ratiba ya Rais waMsumbiji Mhe. Daniel Chapo aliyefanya ziara ya siku tatu ya kiserikali nchini kuanzia Mei 7 Hadi 9 ,2025
Mama Gueta amesema“Hospitali yetu ya Maputo haiwezi kufanya haya yote tunatamani ije ishirikiane na hospitali hii katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo”.
“Tunatamani hospitali kama hii iwepo katika nchi yetu na katika ukanda wa Kusini, Kati na Kaskazini ili iweze kuwahudumia mama, baba, kaka na dada zetu wenye matatizo ya moyo”.
“Tunategemea kutuma ujumbe wetu kuja kujifunza namna ya kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo, tunashukuru sana kwa kuja kwetu nchini Tanzania tumejifunza mengi”
ZINGATIA:-   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inauwezo mkubwa wa kuhudumia wagonjwa wa nje 2,000 na kulaza wagonjwa 100 kwa wiki.