TSH BIL 13.3 KUBORESHA BARABARA, MADARAJA RUFIJI
PWANI
Jumla ya mikataba mitano ya shilingi bilioni 13.3 imesainiwa ili kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Gharama hizo zinahusisha ukarabati wa barabara ya Nyamwage yenye Kilomita 28, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Chumbi- Kiegele yenye kilomita 1.4, ukarabati wa barabara ya Mohoro- Mtanga kilomita 12.3 na Mohoro Ndundutawa yenye kilomita 7.5.
Pia ukarabati wa barabara ya Nyamwage- Mpakani- Nambunju na ujenzi wa barabara za lami katikati ya mji wa Ikwiriri ambapo kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kuiunganisha wilaya hiyo na maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanzania.