MEGAWATI 2,115 ZA JNHPP ZAUNGANISHWA GRIDI YA TAIFA
TANZANIA
Hadi Machi 2025, megawati 2,115 kutoka mradi wa Kufua Umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) zimeunganishwa kwenye gridi ya taifa na kuongeza kiwango cha umeme kufikia megawati 4,031.7.
Zingatia:- mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere umegharimu shilingi trilioni 6.6 na Ujenzi wa mradi huo una uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 kwa siku
MUHIMU:- mwelekeo wa Serikali katika sekta ya nishati kwa mwaka 2025/2026,ni kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme; mradi wa kupeleka nishati ya umeme katika vitongoji vyote Tanzania Bara na miradi ya kielelezo na kimkakati ya mafuta na gesi asilia.
Vilevile, Serikali itaendelea kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na upatikanaji wa nishati ya mafuta vijijini kupitia uanzishwaji wa vituo vya mafuta katika maeneo ya vijijini.