TANZANIA,MSUMBIJI KUSHIRIKIANA BIASHARA,UWEKEZAJI
DAR ES SALAAM
Serikali za Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika biashara na uwekezaji.
Hayo yamesemwa na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Mei 8,2025 Ikulu, Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na kuzungumza na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo ambaye amefanya ziara ya kikazi ya siku tatu nchin (Mei 7-9,2025)
Katika mazungumzo ya uwili wamekubaliana kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo na wa kati ili wafanye biashara kwa urahisi.
Pia MaRais hao wamekubaliana kuharakisha uanzishwaji wa vituo vya pamoja vya mpakani ili kuondoa shida wanazopata wananchi wa pande zote mbili katika kufanyabiashara za kuvuka mipaka.
Vilevile wamekubaliana kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kiuchumi itakayokuwa na jukumu la kufuatilia kwa karibu zaidi ambayo pande zote mbili zimekubaliana ili kukuza uchumi.