SERIKALI KUENDELEZA MABONDE NCHINI
TANZANIA
Serikali inaendelea na mpango wa kuyaendeleza mabonde nchini kwa kuyatumia kutoa huduma za kijamii ikiwemo upatikanaji wa maji na nishati ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na mafuriko.
Katika kutimiza azma hiyo, moja ya mkakati uliochukuliwa na Serikali ni kuunda mamlaka za mabonde zenye wajibu wa kufanya ufuatiliaji wa mwenendo upitishaji maji na kuratibu namna nzuri ya utumiaji wa mabonde hayo.
Miongoni mwa mabonde yaliyoendelezwani pamoja na bonde la mto Rufiji (kwa kuanzisha mradi wa kuzalisha umeme), uchimbaji wa bwawa kubwa ambalo linategemea maji ya mto Ruvu mkoani Morogoro ambapo ujenzi wa mabwawa haya yataleta maslahi kwa Watanzania ikiwemo kwenye sekta za kilimo, nishati, maji na mifugo.