DODOMA YAPOKEA TSH BIL 96.8 UMEME WA REA

DODOMA YAPOKEA TSH BIL 96.8 UMEME WA REA

DODOMA YAPOKEA TSH BIL 96.8 UMEME WA REA

DODOMA
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 96.8 ili kuhakikisha miradi ya umeme vijijini inatekelezwa katika mkoa wa Dodoma na wananchi wanapatiwa huduma ya umeme ili kuwapatia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni ya kutekeleza miradi ilikuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa ili iweze kuwanufaisha wananchi.
Aidha, Mkoa wa Dodoma una jumla ya vijiji 580 ambapo vijiji vyote sawa na asilimia 100 vimepata huduma ya umeme kupitia miradi ya awali kama vile REA awamu ya kwanza (REA I), REA awamu ya pili (REA II), REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza (REA III Round I), na REA awamu ya tatu mzunguko wa pili (REA III Round II).
Jumla ya vitongoji 1,773 na mitaa 225 vimefikiwa na huduma ya umeme kati ya vitongoji 3,212 na mitaa 258 ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni sawa na asilimia 57 ya vitongoji vyote.
Vilevile Wakala unaendelea na utekelezaji wa mradi wa HEPIIA katika vitongoji 150 vya mkoa wa Dodoma kupitia mkandarasi Derm Group Ltd  ambapo hadi kufikia mwezi March 2025, mkandarasi amekwisha kusimamisha nguzo katika vitongoji Vyote.