UWEKEZAJI MKUBWA KUKABILIANA NA VIFO VYA MAGONJWA YA MOYO
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2019 zinaonesha kuwa, takriban watu milioni 17.9 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo ikiwa ni sawa na asilimia 32 ya vifo vyote duniani ikiwemo Tanzania.
kutokana na changamoto hiyo kubwa Duniani Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa kwa kiwango cha kimataifa kwenye vifaa tiba pamoja na mitambo mbalimbali ikiwemo mashine za uchunguzi wa magonjwa kama MRI, CT- Scan pamoja na Ultrasound.
Katika Taasisi hii ya JKCI, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha usimikwaji wa mashine Tatu za Cathlab carto kwa ajili ya upasuaji kwa njia ya tundu dogo ambapo upa suaji huu umepunguza kwa kiwango kikubwa muda wa mgonjwa kukaa hospitali
Pia Serikali imeendelea kuhakikisha Hospitali zinakuwa na uwezo wa kutoa huduma za matibabu kwa wananchi katika namna mbalimbali ikiwemo programu ya tiba mkoba (Outreach Programe) ijulikanayo kwa jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach programe. "Upanuzi wa huduma za kibingwa za matibabu ya magonjwa ya moyo katika hospitali za kanda Chato, Hospitali ya Benjamini Mkapa, Hospitali ya Kanda Mtwara na nyinginezo.
#BimkubwanaAfyaKazini