MADARAJA MATATU YANAJENGWA LINDI

 

MADARAJA MATATU YANAJENGWA LINDI

MADARAJA MATATU YANAJENGWA LINDI

LINDI

Serikali imeanza utekelezaji wa barabara ya Kiranjeranje-Nanjirinji hadi Ruangwa kwa kuanza na ujenzi wa madaraja makubwa matatu yaliyopo katika barabara hiyo yenye jumla ya urefu wa kilometa 120 Mkoani Lindi.
Madaraja hayo ni Daraja la Kigombo lenye urefu wa mita 25 na utekelezaji wake umefikia asilimia 25, Daraja la Nakiu lenye urefu wa mita 70 ambapo Mkandarasi yupo kwenye maandalizi ya ujenzi na  Daraja la Mbwemkuru 3 lenye urefu wa mita 100 ambalo lipo katika hatua ya mapitio ya usanifu.
Aidha,Serikali inaendelea kutafuta fedha ili iweze kujenga barabara ya Kiranjeranje-Nanjirinji hadi Ruangwa hiyo kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa kilometa 120 mkoani humo.