UBORESHAJI MIUNDOMBINU KATIKA HIFADHI
Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 14.99 kwa ajili ya uboreshaji ili kuongeza namna bora ya ufukiaji wa watalii.
MRADI WA MAJI HIFADHI NCAA:- Katika kipindi cha utawala wa Mhe. Rais Dkt Samia jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetolewa kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji katika hifadhi.
UJENZI MAKAO MAKUU NCAA:-Jumla ya shilingi bilioni 10.47 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya NCAA ya Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha.
KUTAMBULIWA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA UTALII DUNIANI (UNWTO):-Mnamo mwaka 2023 Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO), Lenye makao yake makuu Madrid Nchini Hispania lilitoa orodha ya nchi 10 bora duniani ambazo ukuaji katika sekta ya utalii umeongezeka kwa tarakimu mbili katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023.
Katika orodha ya nchi hizo kumi Tanzania ilishika nafasi ya nane kidunia na nafasi ya pili Barani Afrika baada ya Ethiopia kwa ukuaji huo.Nchi zilizopo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Qatar(+95%),Saudi Arabia (+58), Albania (+56%), El salvador (+32) , Armenia (+30%), Ethiopia (+28%), Jordan na Colombia (zote zina +23%), Tanzania (+19), Honduras na Serbia ( zote zina + 17%
#Bimkubwanautaliikazini