SHILINGI TRILIONI 67 ZAWEKEZWA KWENYE MIRADI YA UWEKEZAJI NCHINI
Katika kipindi cha uongozi wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jumla ya shilingi trilioni 67 zimewekezwa katika miradi ya uwekezaji nchini.
Kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) tangu 2021, miradi 2,099 imesajiliwa huku miradi 1,982 ikianzishwa na huku uwekezaji katika sekta ya viwanda ikiongezeka.Katika miradi iliyoanzishwa, miradi ya ubia imefikia 476, miradi iliyohusisha upanuzi wa maeneo ya uwekezaji ni 117, miradi ya Watanzania ni 719 na miradi ya wageni ni 904.
Kwa miradi yote iliyowekezwa nchini, sekta ya viwanda ndiyo inayoongoza kwa uwekezaji na kuanzia 2021 hadi Februari 2025, miradi 951 ya viwanda imesajiliwa.
Miradi hii inatarajiwa kuleta ajira 124,339 na kuwekeza mitaji ya takribani Sh trilioni 27, miradi hii ya viwanda inachukua asilimia 45 ya miradi ya sekta zote iliyosajiliwa katika mwaka 2021 hadi 2025
Aidha, miradi ya viwanda imechukua asilimia 42 ya mitaji ya sekta zote iliyosajiliwa katika kipindi hicho na kufanya miradi ya viwanda kuwa ndiyo sekta inayoongoza sekta zote kwa idadi ya miradi, mitaji na ajira.
Jumla ya miradi 951 ya viwandani imesajiliwa, miradi mipya ya viwandani 917 imeanzishwa, miradi 36 imehusu upanuzi wa viwanda, miradi 244 ya viwanda ni ya Watanzania, imesajiliwa, miradi ya viwandani ya wageni 501 imesajiliwa, miradi ya ubia 206.
ZINGATIA:- Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuvutia uwekezaji ukifuatiwa na Mkoa wa Pwani
#Bimkubwanauwekezajikazini