MHE.RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA PAPA FRANCIS
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole (kwa niaba ya Watanzania) kufuatia taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis kilichotokea jumatatu ya pasaka tarehe 21, April 2025.
Rais Samia ameandika "Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko. Katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko ameishi maisha yake kama mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani"
Dkt Samia ameongeza
"Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote."
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi.
Amina.
Bimkubwa Tanzania tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kutoa pole kwa wote walioguswa na kifo cha Papa Francis.