SIR JIM WA MANCHESTER ATEMBELEA IKULU DSM
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo April 11, 2025 amepokea mgeni ambae ni Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo.
Katika mazungumzo yao Rais Dkt. Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers ambayo ina shughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya vizuri katika kudhibitimuingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
Nae, Sir Jim Ratcliffe amebainisha kuwa Kupitia Taasisi yake ya Six Rivers imedhamiria kurejesha hadhi ya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo.