MBOLEA YA RUZUKU YAONGEZA UZALISHAJI CHAKULA

 

MBOLEA YA RUZUKU  YAONGEZA UZALISHAJI CHAKULA

MBOLEA YA RUZUKU  YAONGEZA UZALISHAJI CHAKULA

DODOMA
Tanzania imefanikiwa kudumisha uwezo wa kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 125, hatua ambayo imechangiwa na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani milioni 20.4 msimu wa kilimo 2022/2023 hadi tani milioni 22.8 msimu wa 2023/2024.
Ongezeko hilo la uzalishaji limetokana na matumizi ya mbolea ya ruzuku inayotolewa kwa wakulima, upanuzi wa mitandao ya kilimo cha umwagiliaji, uboreshaji wa huduma za ugani wa kilimo na matumizi ya mbegu bora.
Aidha upatikanaji wa mbolea nchini umeendelea kuimarika, ambapo hadi kufikia Januari 31, 2025 tani milioni 1.21 zinapatikana ambazo ni sawa na 80.9% ya makadirio ya mahitaji ya kitaifa ya tani milioni 1.5 kwa msimu wa kilimo wa 2024/2025.
Katika msimu huo huo, jumla ya tani 388,619.87 za mbolea ya ruzuku, yenye thamani ya takriban shilingi bilioni 131.66 zilikuwa tayari zimesambazwa kwa wakulima wapatao 4,223,278 nchini kote.