HATUA ZINGINE ZILIZOPIGWA KWENYE ELIMU NDANI YA MIAKA MINNE

 

HATUA ZINGINE ZILIZOPIGWA KWENYE  ELIMU NDANI YA MIAKA MINNE

HATUA ZINGINE ZILIZOPIGWA KWENYE  ELIMU NDANI YA MIAKA MINNE

MIKOPO
(a)KUONGEZA BAJETI YA MIKOPO (Angalia kwenye jedwali hapo juu)
(b) KUONGEZA BOOM KWA WANAFUNZI
Mhe.Rais Dkt Samia kupitia mkutano wake na wanafunzi na viongozi wa jumuiya ya vyuo vikuu TAHLISO Mwaka 2023 aliahidi kuongeza boom kutoka shilingi 8,500 ya wakati huo hadi shilingi 10,000 kwa siku, mpango huu unatekelezwa hadi sasa na hii ni hatua muhimu kwa wanafunzi wanaonufaika na mpango huu.
(c) KUFUTA TOZO YA "VALUERETENTION FEE
Mwezi Mei 2021, Mhe. Rais Samia alitangaza kufuta tozo ya asilimia 6 ya "Value Retention Fee" ambayo ilikuwa ikitozwa wanufaika wa mikopo ya HESLB juu ya deni lao. Hatua hii ilipunguza mzigo wa kifedha kwa wahitimu wanaolipa mikopo yao, ikifanya iwe rahisi kwao kurejesha kiasi walichokopa bila adhabu za ziada.
(d)  KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA JUU: 
Serikali ya awamu ya sita imefanikisha upanuzi wa vyuo vikuu katika mikoa ambayo hapo awali haikuwa na taasisi za elimu ya juu.Hatua  hii inatekelezwa kupitia miradi HEET (Higher Education for Economic Transformation), ambayo inafadhiliwa na Benki ya Dunia 
(e)  MIKOPO VYUO VYA KATI, DIPLOMA
Mwaka 2023 Serikali ya Tanzania chini ya Mhe Rais Dkt Samia  ilipendekeza kuwapa mikopo wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na vyuo vya kati watakaosoma fani za kipaumbele kama vile sayansi, afya pamoja na elimu kuanzia Julai 2023.
Katika mwaka wa masomo 2023/24 jumla ya wanafunzi 8,000 wamenufaika na mpango huu huku kiasi cha shilingi bilioni 48 kimetumika katika mpango huo na kwa mwaka wa masomo 2024/25 serikali inawapatia ahueni wanafunzi wapatao 10,000 wa fani za kipaumbele wa vyuo vya kati ngazi ya diploma (stashahada)  ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wake wa kuongeza fursa za mafunzo ya amali inayohusisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
MUHIMU:- Hatua hii  ni miongoni mwa mabadiliko ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na mtaala ulioboreshwa ambao ulizinduliwa rasmi na Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari 2025.
#Bimkubwakazininaelimu