KUTANGAZWA NA UNWTO KUWAMJUMBE WA BARAZA TENDAJIKUPITIA MKUTANO ULIOFANYIKA UZBEKISTAN.
Mwishoni mwa mwezi septemba 2023 UNWTO imeitanganza Tanzania kuwa MJUMBE WA BARAZA TENDAJI LA SHIRIKA hilo ulimwenguni maamuzi ambayo yalipitishwa kwenye mkutano wake mkuu wa 25 kwenye mkutano uliofanyika nchini Uzbekistan.
SERENGETI KUWA HIFADHI BORA KWA MIAKA MINNE MFULULIZO BARANI AFRIKA.
Kwa mara ya nne mfululizo, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania imeibuka kuwa Hifadhi bora ya Safari ya Afrika kutokana na utafiti uliofanywa mwaka 2023 kupitia Safari-Bookings.
Soma hapa orodha na kwenye mabano ni alama iliyopata hifadhi kati ya alama 5 zilizowekwa kama kigezo :-
Hifadhi ya Kitaifa ya Serengeti, Tanzania (4.87), Hifadhi ya Kibinafsi ya Sabi Sand, Afrika Kusini (4.71), na Hifadhi ya Kitaifa ya Luangwa Kusini, Zambia (4.71).
Mbuga zingine ni Okavango Delta, Botswana (4.70), na Kgalagadi Transfrontier Park, Afrika Kusini (4.67). Mbuga 200 kutoka nchi 15 za Afrika zilijumuishwa katika utafiti huo (Botswana, Eswatini (zamani Swaziland), Ethiopia, Lesotho, Kenya, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia, na Zimbabwe.
#Bimkubwanautaliikazini