MASHINE 100 ZA KUSAFISHA FIGO ZASAMBAZWA NCHINI

MASHINE 100 ZA KUSAFISHA FIGO ZASAMBAZWA NCHINI

MASHINE 100 ZA KUSAFISHA FIGO ZASAMBAZWA NCHINI 

TANZANIA

Serikali imesambaza mashine zaidi ya 100 pamoja na vitendanishi katika hospitali za rufaa za mikoa mbalimbali ili kupunguza gharama za matibabu ya kusafisha figo nchini.Pamoja na usambazaji wa mashine hizo, serikali pia imeongeza vituo vya kutoa huduma ya dialysis katika hospitali 15 za rufaa za mikoa na hospitali zote za kanda, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi wengi zaidi.

Aidha, Katika kuhakikisha ushindani wa bei na upatikanaji wa vifaa tiba, serikali ina mpango wa kuongeza wadau na taasisi zinazohusika na uingizaji wa vitendanishi, dawa na vifaa tiba vinavyotumika kwenye huduma hiyo, badala ya kuruhusu kampuni au taasisi moja kutawala soko.

ZINGATIA:- Hatua hizi ni sehemu ya jitihada za serikali kuboresha huduma za afya na kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana kwa gharama nafuu kwa Watanzania wote.