HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MAGHARIBI WILAYA YA UJIJI MKOANI KIGOMA.
Serikali katika mwaka wa fedha 2024/25 imetenga kiasi cha fedha Sh. bilioni nne kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi wilaya ya Ujiji mkoani Kigoma ambayo inajengwa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Katika awamu ya kwanza ya mradi huo wa ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi - Kigoma unahusisha jengo la wagonjwa wa nje na huduma ya dharura-OPD/EMD Complex, Jengo la huduma za uchunguzi na utambuzi wa magonjwa -Diagnostic Service Complex, ujenzi wa jengo la huduma za Dawa – Pharmaceutical Services Block, jengo la Upasuaji - Surgical Complex, jengo la Mama na Mtoto- Maternity Complex.
Pia majengo mengine ni jengo la Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumuIntensive Care Unit Block,jengo la utawalaAdministration Complex, jengo la kutakasia vifaa tiba- Central Sterile Supply Department (CSSD), jengo la kufulia- Laundry,jengo la kuhifadhia Maiti- Mortuary,jengo la kuchomea taka hatarishiIncinerator,uzio, njia za kupita wagonjwa na mazingira ya nje
#BimkubwanaAfyakazini