HATUA ZILIZOPIGWA KWA MIAKA MINNE YA MHE. RAIS SAMIA KWENYE WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
KUPUNGUZA IDADI YA MAKOSA MAKUBWA YA JINAI
Serikali imefanikiwa kupunguza idadi ya makosa makubwa ya jinai yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi kutoka 45,485 hadi 43,146
b. KUUNGANISHA VITUO VYA POLISI NA MKONGO WA TAIFA HADI KUSOMANA
Serikali imefanikisha kusomana mfumo wa kielektroniki wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama na Vituo vikuu vya Polisi katika mikoa 23 vilivyo unganishwa na Mkongo wa Taifa
c. KUPUNGUZA MLUNDIKANO WA WAFUNGWA NA MAHABUSU MAGEREZANI
Pamoja na mambo mengine, serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kupunguza mlundakano wa Wafungwa na mahabusu waliokuwa magerezani kutoka wafungwa 38,501 mwaka 2019/2020 hadi 27,461 mwaka 2024
d. KUTEKELEZA MPANGO WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA MAGEREZANI
Katika kipindi cha uongozi wa Mhe Rais Dkt Samia, serikali kupitia Jeshi la Magereza limetekeleza programu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia ya Miaka 3 ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 35.44 kinatumika kwenye mpango huo.
#bimkubwanamamboyandanikazini