HATUA ZILIZOPIGWA KWAMIAKA MINNE YA MHE. RAIS SAMIA KWENYE WIZARA YA NDANI YA MAMBO YA NCHI
UTEKELEZAJI WA MIJI SALAMA (SAFER CITIES)
Mradi umeanza kutekelezwa 2024/25 Arusha,Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza
ambapo kamera 6500 za Teknologia ya Akili Bandia zitafungwa katika maeneo mbalimbali
⦁ UIMARISHAJI MATUMIZI YA TEHAMA
Serikali katika kipindi cha miaka minne imeendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji haki kwa kuimarisha mifumo ya kielektroniki ya usikilizaji wa mashauri, utunzaji wa kumbukumbu, ukusanyaji wa takwimu na utoaji wa taarifa za kimahakama unaofahamika kama JUDICIAL STATISTICAL DASHBORD SYSTEM pamoja na matumizi ya Video Conference katika
kuendesha mashauri ya usuluhishi ya kimataifa na hata baadhi ya mashauri ya ndani.
Aidha, Mahakama imeanza majaribio ya matumizi ya teknolojia ya akili mnemba ya kunakili na kutafsiri lugha ya mawasiliano wakati wa mwenendo wa usikilizwaji wa mashauri mahakamani.
#bimkubwanamamboyandanikazini