JUZUU MPYA ZA SHERIA KURAHISIHA MAAMUZI MAHAKAMANI
DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema juzuu mpya za toleo la Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu la mwaka 2023 zitasaidia katika kurahisisha maamuzi mahakamani,kuongeza uwazi hatua ambayo itaongeza kujenga imani ya wananchi kwa serikali yao.
Akizungumza mara baada ya kutia saini Tamko la kuzindua Toleo la Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu la mwaka 2023 kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha Sheria ya urekebu wa sheria Dkt Samia amesema
" kwa upande wa mahakama tunatazamia itapunguza muda unaotumika kwenye kufanya utafiti ili kupata uhakika wa sheria inavyosema na hivyo kurahisisha maamuzi"
Dkt Samia ameongeza "Juzuu hizi za sheria zilizorekebishwa ni muhimu sana katika kuongeza uwazi na kuzidi kujenga imani ya wananchi kwa serikali yao,aidha ni nyenzo muhimu itakayosaidia kupunguza matumizimabaya yamadaraka"
ZINGATIA:- ZOEZI LA UZINDUZI WA UREKEBU WA SHERIA UMEJUMUISHA SHERIA ZOTE ZILIZOTUMIKA KUANZIA MWAKA 2003 HADI DESEMBA 2023 NA SHERIA ZOTE KUU 446 ZIMEHUSISHWA KWENYE MABADILIKO HAYA YALIYOZINDULIWA APRIL 23,2025
