HATUA ZILIZOPIGWA KWA MIAKA MINNE YA MHE. RAIS SAMIA KWENYE WIZARA YA NDANI YA MAMBO YA NCHI
MAGARI KWA AJILIYA UTAWALA NA UKAGUZI
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepokea magari 28 kati ya hayo 15 ni shughuli za utawala na ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya moto na magari 13 ya kuzima moto na uokoaji .
KUANZISHA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA
Kampeni hii inafanyika kwa miaka mitatu kuanzia mwezi Machi, 2023 hadi mwezi Februari, 2026 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kampeni imejikita katika kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi hususan katika masuala ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala, na masuala yahusuyo haki za binadamu kwa ujumla.
Utekelezaji wa kampeni unafanyika kwa kushirikiana na Wizara na Taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia, Wanazuoni na Wadau wa Maendeleo. Lengo kuu la Kampeni hii ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini.
Matokeo ya muda mrefu wa Kampeni hii ni kuchangia katika kuboresha upatikanaji wa haki kwa watu wasiojiweza, hususan wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi.
Hadi hivi sasa kupitia kampeni hiyo ambayo inatolewa bure imefanikiwa kuwafikia zaidi ya wananchi milioni moja wakiwemo wanawake 681,326 na wanaume 691,773 katika mikoa 19 nchini. Pamoja na kampeni hiyo, Rais Dkt. Samia amefanya mageuzi makubwa na kuweka kipaumbele katika kutatua changamoto zilizopo sekta ya huduma za sheria nchini.
#bimkubwanamamboyandanikazini