MABEHEWA 264 YA MIZIGO TRC KUANZA KAZI

 

MABEHEWA 264 YA MIZIGO TRC KUANZA KAZI

MABEHEWA 264 YA MIZIGO TRC KUANZA KAZI

TANZANIA
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limekamilisha majaribio ya mabehewa 264 ya reli ya Standard Gauge (SGR) ikiwa ni hatua kubwa kuelekea kuanza kwa usafirishaji wa mizigo katika reli ya kisasa.
Mabehewa hayo yaliwasili nchini Desemba 2024, na majaribio yake yalifanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) ambapo mchakato huo ulihusisha tathmini za uthabiti katika hali ya kusimama na kusonga ili kuhakikisha kwamba mifumo yote muhimu, ikiwa ni pamoja na kufunga breki kwenye mikunjo, inafanya kazi ipasavyo.
Kati ya mabehewa 264 yaliyojaribiwa, 200 yameundwa kwa usafirishaji wa makontena, huku 64 yakilengwa kubeba mizigo mizito. 
Aidha mabehewa hayo yanakidhi viwango vinavyotakiwa, yakiwa na mwendo wa kasi wa hadi kilomita 120 kwa saa.
Hatua inayofuata inahusisha LATRA kutoa uthibitisho rasmi kwa TRC, kama inavyotakiwa na sheria, kuidhinisha mabehewa hayo kuanza shughuli za usafirishaji wa mizigo.
KUMBUKA:- Mabehewa haya ni sehemu ya jumla ya mabehewa 1,430 yanayotengenezwa na kampuni ya Kichina ya CRRC kwa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha sekta ya usafirishaji wa mizigo nchini kupitia reli ya SGR.