TSH MIL 235.5 ZAJENGA MAABARA 2 ZA KOMPYUTA TANGA

 

TSH MIL 235.5 ZAJENGA MAABARA 2  ZA KOMPYUTA TANGA

TSH MIL 235.5 ZAJENGA MAABARA 2  ZA KOMPYUTA TANGA

TANGA
Seriakli kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imezindua maabara mbili za kompyuta zenye vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Sh milioni 235.5 katika Shule ya Sekondari Magamba na Shule ya Msingi Shukilai, wilayani Lushoto, Tanga.
Maabara hizo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 (toleo la 2023), inayosisitiza matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.
Kupitia programu hiyo shule zimepewa kompyuta 26, monitor 26, projekta moja, mashine ya kurudufu maandishi, madawati na vifaa vingine vya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).
Mradi huo umefanikishwa kwa ushirikiano kati ya TET na Korea Kusini kupitia programu ya KLIC (Korean e-Learning Improvement Cooperation).