TSH BIL 11.4 ZAJENGA BWAWA LA KASORI
SIMIYU
Serikali imekamilisha ujenzi wa Bwawa la Kasori Mkoani Simiyu kwa gharama ya shilingi bilioni 11.4
Bwawa hilo linatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wakulima wa Mkoa huo, hususan katika umwagiliaji na uhifadhi wa maji kwa ajili ya kilimo cha pamba na mazao mengine.
Katika msimu uliopita, jumla ya tani 70,000 za pamba zilizalishwa lakini baada ya uwepo wa bwawa hilo, mkoa unatarajia kuzalisha tani 200,000.
Aidha, Serikali imeanza ujenzi wa nyumba sita za maafisa ugani katika wilaya za Bariadi na Meatu katika kuhakikisha kuwa wataalamu wa kilimo wanakuwa karibu na wakulima kwa ajili ya kuwapa ushauri na msaada wa kitaalamu.