TSH MIL 100 ZA DKT SAMIA ZAWAGUSA WENYE SHIDA YA MOYO
DODOMA
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita jumla ya shilingi milioni 100 zimetolewa kutoka kwenye mfuko maalumu wa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kusaidia kupunguza gharama (kiasi cha shilingi milioni 562) za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua kwa wagonjwa 60 kati ya hao watoto 38 na watu wazima 22 katika hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma.
Aidha, wataalamu wa hospitali hiyo, wamefanikiwa kufanya uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa wagonjwa 1,173, upandikizaji betri wagonjwa 23, kuweka vizibua njia ya mishipa ya moyo kwa wagonjwa 42.
MUHIMU:- Hospitali ya Benjamin Mkapa inatarajia kuanza kutumia roboti kwa upasuaji ndani ya miaka mitatu ijayo ili kuongeza usahihi wa matibabu.
