SERIKALI YALIPA TSH TRIL 2.3 BIMA YA AFYA

 

SERIKALI YALIPA TSH TRIL 2.3 BIMA YA AFYA

SERIKALI YALIPA TSH TRIL 2.3 BIMA YA AFYA

TANZANIA
Serikali imelipa Shilingi Trilioni 2.3 kwa vituo vya afya ili kugharamia huduma za bima ya afya, hatua inayoonesha jitihada za kuimarisha upatikanaji wa matibabu kwa wananchi.
Lengo la Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na bima ya afya ili kupata huduma za matibabu kwa uhakika hivyo ili kufanikisha hilo, mwaka 2023, Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alisaini Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote itakayowezesha kila Mtanzania kupata huduma ya afya bila kujali hali ya kiuchumi.