KITUO CHA UFUGAJI SAMAKI CHAJENGWA CHATO

 

KITUO CHA UFUGAJI SAMAKI CHAJENGWA CHATO

KITUO CHA UFUGAJI SAMAKI CHAJENGWA CHATO

GEITA
Serikali inaendelea na ujenzi wa kituo kikubwa cha ufugaji samaki katika Kijiji cha Rubambangwe, wilayani Chato, mkoani Geita. 
Mradi huo unagharimu jumla ya shilingi bilioni tatu, ambapo awamu ya kwanza iligharimu shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanzisha mradi, na awamu ya pili inatarajiwa kukamilisha mradi kwa kiasi kingine cha shilingi bilioni 1.5.
Kituo hiki kinatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya uvuvi nchini kwa kutoa suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wafugaji wa viumbe maji katika kanda ya Ziwa Viktoria, hususan katika maeneo ya Rubambangwe na maeneo jirani. 
Mradi huu unalenga kuongeza uzalishaji wa samaki na kuboresha shughuli za uvuvi nchini.
Aidha, mradi huu ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhamasisha, kuendeleza, na kusimamia ufugaji samaki wenye tija katika ukanda wa Ziwa Victoria.