TSH BIL 22.27 KUWEKA LAMI KM 10.1 SONGEA
RUVUMA
Katika jitihada za kuboresha miundombinu ya barabara mkoani Ruvuma, Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 10.1 kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Songea.
Mradi huo unafadhiliwa na mpango wa TACTIC kupitia Benki ya Dunia,katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika mji wa Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Hadi sasa, mradi umekamilika kwa asilimia 87.53 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo tarehe 8 Juni 2025 ambapo kwa kukamilika kwa mradi huu Wananchi wa Songea wanatarajia kupata manufaa makubwa kutoka kwa mradi huu, ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za usafirishaji, kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu, na kuboresha biashara na uchumi wa mji wa Songea.