WADAU NA WB WAIPONGEZA TZ UPATIKANAJI UMEME

 

WADAU NA WB WAIPONGEZA TZ  UPATIKANAJI UMEME

WADAU NA WB WAIPONGEZA TZ  UPATIKANAJI UMEME

DAR ES SALAAM

WADAU wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia wameipongeza Tanzania kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa wote.

Pongezi hizo zimetolewa  na Raisi wa benki ya dunia Bw. Ajay Banga,Rais wa benki ya mendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Akinwumi Adesina na Rais wa Wakfu wa Rockefeller Dk Rajiv Shah leo janauri 28, 2025 kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika  kuhusu nishati unaofanyika kwa siku mbili nchini Tanzania ( Januari 27 na 28) Jijini Dar es slaam.

Wametaja hatua ya Tanzania kuingiza vijiji vyake kwenye gridi ya Taifa na jitihada  za kufikisha umeme katika vijiji vyote huku hatua za kufikisha huduma hiyo kwenye vitongoji zikichagiza pongezi hizo.

Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, ameeleza kufurahishwa kwake na mafanikio ya Tanzania, na kupongeza jitihada za serikali za kusambaza umeme maeneo ya vijijini na mijini, kuwezesha wananchi kukuza uchumi wao kwa kuzingatia hali ya uhakika. 


"Tanzania inatumika kama kinara na mwanga kwa wengine kufuata. Ingawa wana mipango kabambe ya siku zijazo, lazima tuwapongeze kwa yale ambayo tayari wamekamilisha, "alisema Bwn Banga.

 Nae Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Akinwumi Adesina pia ameipongeza Tanzania kwa maendeleo yake ya kuvutia katika kusambaza umeme vijijini.

Adesina ameeleza kuwa mataifa mengine ya Afrika yanaweza kujifunza kutokana na mafanikio ya Tanzania katika kuimarisha upatikanaji wa umeme.

Hatuwezi kujiendeleza gizani,” Dk Adesina amesema huku akirejea wito wa Banga wa kuongeza ushirikiano.

Aidha Rais wa Wakfu wa Rockefeller Dk Rajiv Shah amesema kuwa kufikia lengo kubwa la upatikanaji wa nishati kwa Afrika kutahitaji ushirikiano katika sekta ya umma na ya kibinafsi.

"Hatua ya kufikia upatikanaji wa umeme kwa wote barani Afrika lazima iwe mchakato unaoongozwa na Waafrika," amehitimisha.


ZINGATIA:- Mpango huo unalenga kuhakikisha kuwa mataifa yote ya Afrika, kupitia Mkataba wa Nishati, yanaweka malengo yanayoweza kufikiwa kuelekea lengo la kuunganisha watu milioni 300 na umeme ifikapo 2030.