BARABARA YA KIMARA - BONYOKWA - KINYEREZI (7KM) KUJENGWA

BARABARA YA KIMARA - BONYOKWA - KINYEREZI (7KM) KUJENGWA

BARABARA YA KIMARA - BONYOKWA - KINYEREZI (7KM) KUJENGWA

DAR ES SALAAM
Serikali kupitia wizara ya ujenzi inajenga barabara ya Kimara - Bonyokwa - Kinyerezi yenye urefu wa kilometa 7, mkoani Dar es Salaam.
Ujenzi wa barabara hiyo utajumuisha daraja lenye mita 25 na madaraja madogo saba ya kalvati na mradi huo unatekelezwa na mkandarasi mzawa Nyanza Road Works.
Barabara hiyo muhimu inatarajiwa kuwa kiunganishi kikubwa kati ya majimbo ya Ubungo na Segerea, hatua inayotarajiwa kuboresha huduma za usafiri na kuinua uchumi wa eneo hilo.