TSH BIL 45.6 KUBORESHA MIUNDOMBINU KAGERA

 

TSH BIL  45.6 KUBORESHA MIUNDOMBINU  KAGERA

TSH BIL  45.6 KUBORESHA MIUNDOMBINU  KAGERA

KAGERA
Serikali ya Awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ushirikiano wa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mpango dharura (CERC PROJECTS), imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 45.6  kwa ajili ya kutekeleza miradi mitano ya miundombinu ya barabara katika mkoa wa Kagera.
Miradi hiyo ni pamoja na Daraja la Kyanyabasa (mita 105), Daraja la Kalebe (mita 60), Daraja la Kamishango (mita 45),Daraja la Kyetema (mita 45) na Daraja la Kanino (mita 30) pamoja na barabara unganishi ambazo zinatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Miradi hiyo ya  dharura inatekelezwa kwa miezi 12 na kukamilika kwa miradi hiyo ya dharura kutasaidia wananchi wa Bukoba mjini na vijijini kupita kwenye madaraja hayo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Utekelezaji wa miradi hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha miundombinu ya usafiri na kuhakikisha maendeleo endelevu kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Tunapatikana Instagram,Facebook,X, TikTok, YouTube:-BimkubwaTanzania.